
MIRUNDIKO YA TAKA NAROK YAZUA HOFU KWA WAKAAJI. Imewalazimu wakaaji wa jijini Narok kuichukulia hali hii ya kuzungukwa na taka kawaida, kwani wametoa malalamishi yao kwa baraza la kaunti hii inayohusika na ukusanyaji wa taka bali ikawa bidii zao zimeambulia patupu. Hakuna wa kushughulika. Ni jambo la kutatanisha kwamba hata ingawa jiji hili la Narok ni lenye kazi sana,kiwango au urari wa uchafu wake umezidi ule wa maeneo ya mashinani katika kaunti hii. Kusongamana kwa watu ndio, kunachangia kuwepo kwa taka nyingi lakini pia kwa kuwajibika taka hizo zaweza kushughulikiwa kwa ufanisi ili kuzingatia usafi ambao ni muhimu zaidi ya mambo yote. Hali inayozua hofu zaidi na kuhatarisha afya ya wakaaji wa jiji na nje ya Narok ni kwamba hakuna hata angalau mapipa ambapo wanaweza tia taka zao. Hii inasababisha kusambaa kwa taka kila mahali,mitaro na hata barabara huwa mapipa yao. La kuhuzunisha pia ni kwamba hakuna atakayezoa taka hizo hapo, ni kazi ya maji ya mvua kubeba taka taka hizo h...