
CHUO KIKUU CHA MOI: URITHI WA KUMKUMBUKA RAIS MOI. Chuo kikuu cha Moi kilianzishwa mnamo mwaka wa 1984 kutokana na pendekezo la jopokazi lililoteuliwa na Mstaafu Rais Daniel arap Moi na kuongozwa na Dkt. Mackay, msomi kutoka Nchini Canada. Jopokazi hili liliandika waraka wa pendekezo kuhusu haja ya kuwa na Chuo kikuu cha pili Nchini Kenya. Ilikuwa sehemu ya ndoto ya Rais Mstaafu Moi kuwa na taasisi za elimu ya juu zikihamishwa kutoka maeneo ya mjini na ndio maana akaanzisha chuo kikuu cha Moi katika eneo la Kesses ambalo lipo kilomita 35 kutoka mji wa Eldoret. "Taasisi hii mpya inapaswa kuanzishwa katika sehemu ya nchi mbali na mji mkuu ", inasoma ripoti ya Mackay ambayo iliweka msingi wa kuanzishwa kwake.Rais Daniel arap Moi alichangia pakubwa kwa kuimarisha Chuo Kikuu cha Moi kwa kutoa shamba hekari 3000 kwa ajili shughuli zake,kujengwa kwa Shule ya Sayansi ya Habari na hata maktaba ya kisasa ya Margaret Thatcher. Shule ya Sayansi ya Habari. Ku...