CHUO KIKUU CHA MOI: URITHI WA KUMKUMBUKA RAIS MOI.


Chuo kikuu cha Moi kilianzishwa mnamo mwaka wa 1984 kutokana na pendekezo la jopokazi lililoteuliwa na Mstaafu Rais Daniel arap Moi na kuongozwa na Dkt. Mackay, msomi kutoka Nchini Canada. Jopokazi hili liliandika waraka wa pendekezo kuhusu haja ya kuwa na Chuo kikuu cha pili Nchini Kenya.

Ilikuwa sehemu ya ndoto ya Rais Mstaafu Moi kuwa na taasisi za elimu ya juu zikihamishwa kutoka maeneo ya mjini na ndio maana akaanzisha chuo kikuu cha Moi katika eneo la Kesses ambalo lipo kilomita 35 kutoka mji wa Eldoret. "Taasisi hii mpya inapaswa kuanzishwa katika sehemu ya nchi mbali na mji mkuu ", inasoma ripoti ya Mackay ambayo iliweka msingi wa kuanzishwa kwake.Rais Daniel arap Moi alichangia pakubwa kwa kuimarisha Chuo Kikuu cha Moi kwa kutoa shamba hekari 3000 kwa ajili shughuli zake,kujengwa kwa Shule ya Sayansi ya Habari na hata maktaba ya kisasa ya Margaret Thatcher.

   Shule ya Sayansi ya Habari.
Kutokana na uhaba wa wataalamu katika kitivo cha mawasiliano na teknolojia, Shule ya Sayansi ya Habari ilianzishwa mnamo mwaka wa 1988. Hapo awali, Wakenya walipotaka kusomea taaluma hii ya Sayansi ya Habari walilazimika kusomea nje ya Kenya na kuenda nchi kama vile Botswana, Namibia na Ghana. Serikali ya Hayati Rais Moi iliagiza kujengwa kwa Shule ya Sayansi ya Habari ili kuziba uhaba huo.

Shule hii ni miongoni mwa shule bingwa chuoni Moi na ipo mkabala wa maktaba ya Margaret  Thatcher (MTL).

      Maktaba ya Margaret Thatcher. 
Katika ziara yake Nchini Kenya, mnamo mwaka 1985,aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza,  Bi. Margaret Thatcher,  alianzisha mchakato wa kujenga maktaba katika Chuo Kikuu cha Moi ambayo inaitwa Margaret Thatcher Library (MTL). Maktaba hii ni ya kipekee katika jimbo la Afrika Mashariki. Serikali ya uingereza ilifadhili ujenzi wa maktaba hii  ya kisasa. Hii ilitokana na uhisiano mzuri uliokuwepo kati ya Kenya na Uingereza. Serikali ya Kenya ilikuwa chini ya uongozi wa Hayati Rais Daniel arap Moi.
Sehemu ya jengo la Maktaba ya Margaret Thatcher katika Chuo Kikuu Cha Moi lililojengwa na 'Triad Consultancy Agencies 'mnamo mwaka wa 1985.Kando  yake ni Shule ya Sayansi ya Habari.  Picha/Google/Chuo Kikuu Cha Moi.


Ni dhahiri shahiri kwamba anapotupa mkono wa buriani Mstaafu Rais Moi,Chuo Kikuu cha Moi kitaishi kuwa na kumbukumbu zake daima dawamu.

Comments

  1. Kiswahili ndio inanisumbua lakini it's a nice article

    ReplyDelete
  2. Chopokazi * jopokazi.
    Historia Safi na kuntu Dada.

    ReplyDelete
  3. Jopokazi* si chopokazi. Kiswahili Chako ki mwafaka ijapokuwa ningependekeza umtaje Rais Mstaafu Daniel Moi Kama mwendazake tangu mwanzo Hadi mwisho

    ReplyDelete
  4. ChopoKazi sio jopokazi lakini umefanya kazi nzuri

    ReplyDelete

Post a Comment

Leave a comment

Popular posts from this blog

MOTHERLAND