LIKIZO YAFANYA WANAFUNZI KUANZA BIASHARA.

Na Lydia Omaya.

Serikali imelazimika kurefusha likizo ya wanafunzi haswa wale wa shule za misingi na upili hadi mwaka ujao kufuatia janga la Corona humu nchini. Vyuo vikuu huenda vitafunguliwa mwezi Septemba ikiwa vitaweza kuzingatia mwongozo utakaotolewa na serikali. Hali hii inatatanisha lakini wanafunzi hawana bidii kusalimu amri na kukaa nyumbani.

Huenda jambo hili la likizo lisionekane kuwa pigo kubwa kwa wanafunzi wa chuo lakini ukweli ni kuwa wameathirika pakubwa. Wamechoshwa na nyumbani. Wengi wameanzisha biashara angalau wapate kujikimu kimaisha.
Agizo la kukaa nyumbani kwa muda zaidi kutoka kwa serikali limesambaratisha ndoto za wanafunzi wengi. Kuna wale waliotarajia kupiga hatua ya masomo lakini sasa hawana budi kusubiri. Kuna wale waliokuwa karibu kutamatisha, imewalazimu kukaa nyumbani.

"Hatuwezi kukaa nyumbani na kuosha mikono tu. Baadhi ya mipango yetu imeharibiwa, "dada Lydiah Mong'ina  ambaye ni mfanyabiashara na mwanafunzi alizungumza. "Hii likizo imehairisha kila kitu,kumaliza kwetu kwa masomo,kupata ajira na hata kuolewa, tutazeekea kwa baba zetu," alimalizia. Hili linaonyesha kuwa wanafunzi wengi hawawezi ngoja elimu yao kuwapa ajira walivyotajaria hapo awali, kwani ngoja ngoja huumiza matumbo ndiposa wamechukua hatua ya kujitafutia ajira.
Mwanafunzi akifanya biashara ya kuuza nyanya Keroka,kaunti ya Kisii.


Wazazi wamekiri kwamba mahitaji ni mengi wanayokuwa nayo watoto wao haswa wa vyuo na mara nyingi huwa wanawategemea wanapokuwa shuleni kukirimia mahitaji hayo. Itakuwa vigumu kuyapata sasa ikiwa wataketi nyumbani tu kwa sababu hakuna pesa wanazopokea toka kwa wazazi.
Wanafunzi wengine wanajihusisha na biashara ili kutafuta karo na pesa za matumizi shuleni siku za usoni na hivyo basi kwao hii ni nafasi inayowafaa sana. Wazazi wengi wamewaanzishia watoto wao biashara na wengine kujiunga na biashara zao ili kufanikisha lengo la kutafuta karo na hata kodi shuleni.

Hali hii ya biashara inazua hofu hata ingawa inafaidi wanafunzi kwa njia moja au nyingine kwa sababu itakuwaje likizo ikimalizika na wasione haja ya kuridi shuleni tena? Litakuwa jambo gumu kwa vile idadi ya wanafunzi kuacha shule itaongezeka na hiyo ni ishara ya hatari kubwa kwa siku zijazo.

Comments

Popular posts from this blog

MOTHERLAND