
LIKIZO YAFANYA WANAFUNZI KUANZA BIASHARA. Na Lydia Omaya. Serikali imelazimika kurefusha likizo ya wanafunzi haswa wale wa shule za misingi na upili hadi mwaka ujao kufuatia janga la Corona humu nchini. Vyuo vikuu huenda vitafunguliwa mwezi Septemba ikiwa vitaweza kuzingatia mwongozo utakaotolewa na serikali. Hali hii inatatanisha lakini wanafunzi hawana bidii kusalimu amri na kukaa nyumbani. Huenda jambo hili la likizo lisionekane kuwa pigo kubwa kwa wanafunzi wa chuo lakini ukweli ni kuwa wameathirika pakubwa. Wamechoshwa na nyumbani. Wengi wameanzisha biashara angalau wapate kujikimu kimaisha. Agizo la kukaa nyumbani kwa muda zaidi kutoka kwa serikali limesambaratisha ndoto za wanafunzi wengi. Kuna wale waliotarajia kupiga hatua ya masomo lakini sasa hawana budi kusubiri. Kuna wale waliokuwa karibu kutamatisha, imewalazimu kukaa nyumbani. "Hatuwezi kukaa nyumbani na kuosha mikono tu. Baadhi ya mipango yetu imeharibiwa, "dada Lydiah Mong'ina ambaye ni mfanyabi...